Nani anaruhusiwa kufanya shughuli za uvuvi katika Ukanda wa Uchumi wa Bahari (EEZ) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Nani anaruhusiwa kufanya shughuli za uvuvi katika Ukanda wa Uchumi wa Bahari (EEZ) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Meli za uvuvi za kigeni na za kitaifa zinaruhusiwa kufanya shughuli za uvuvi katika EEZ ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (URT) mradi tu zinakidhi vigezo na masharti ya leseni ya uvuvi iliyoainishwa katika sheria inayoongoza shughuli za uvuvi katika EEZ. Idara za Uvuvi zinasimamia shughuli za uvuvi katika eneo la bahari katika wizara zinazohusika na uvuvi Tanzania Bara na Zanzibar. Katika hali ya kawaida, hakuna meli ya kigeni inaruhusiwa kufanya shughuli za uvuvi wa kibiashara katika maeneo ya maji ya URT.