Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu

(DSFA)

Ukaguzi wa Ndani

Kushauri juu ya utoshelevu wa udhibiti wa ndani wa Mamlaka.
Kitengo hiki kitafanya shughuli zifuatazo:
(i) Kuandaa na kutekeleza taratibu za ukaguzi kwa mujibu wa viwango vinavyokubalika;
(ii) Kupitia na kutoa taarifa juu ya mifumo iliyopo inayotumika kulinda mali na kuthibitisha kuwepo kwa mali hizo;
(iii) Kupitia na kutoa taarifa kuhusu uendeshaji au programu ili kuhakikisha ulinganifu na malengo na malengo yaliyokusudiwa;
(iv) Kutathmini usimamizi wa vihatarishi vya Mamlaka na kushauri ipasavyo;
(v) Kuratibu ukaguzi wa kisheria kwa kushirikiana na wakaguzi wa nje;
(vi) Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na maalum kadri itakavyohitajika;
(vii) Kupitia na kutoa taarifa juu ya udhibiti sahihi wa ndani wa upokeaji, uhifadhi na matumizi ya rasilimali zote za fedha;
(viii) Kupitia na kutoa taarifa kuhusu ulinganifu wa taratibu za fedha na uendeshaji zilizowekwa katika sheria yoyote au kanuni nyingine yoyote au maelekezo yaliyotolewa chini ya sheria hiyo na taratibu nzuri za uhasibu; na
(ix) Kupitia na kutoa taarifa juu ya utoshelevu wa udhibiti unaojengwa katika mifumo ya kompyuta iliyopo.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo