Kitengo cha TEHAMA 
                        
                    
                
            
                            Kitengo cha TEHAMA 
                        
                    Kutoa huduma za TEHAMA ili kusaidia shughuli za mamlaka.
Kitengo hiki kitafanya shughuli zifuatazo:
(i) Kuanzisha na kutekeleza mkakati wa habari na teknolojia;
(ii) Kuendeleza na kuratibu Habari na Teknolojia jumuishi;
(iii) Kudumisha na kuhuisha vifaa na programu;
(iv) Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala yote ya habari na teknolojia;
(v) Kupeleka miundombinu ya kisasa ya habari na teknolojia;
(vi) Kuimarisha usalama wa mtandao;
(vii) Kuhakikisha upatikanaji wa taarifa na teknolojia kwa njia ya simu na kwa mtandao;
(viii) Kuhakikisha upatikanaji wa taarifa kwa wakati; na
(ix) Kuimarisha usimamizi wa data na maarifa.