Kitengo cha Huduma za Sheria
Kitengo cha Huduma za Sheria
Kutoa huduma za kisheria kwa Mamlaka.
Kitengo hiki kitafanya shughuli zifuatazo:
(i) Kutoa ushauri wa kisheria kuhusu uandishi, madai na mkataba;
(ii) Kupitia na kupendekeza marekebisho ya sheria, kanuni na miongozo;
(iii) Kuiwakilisha Mamlaka katika vyombo vya sheria na usuluhishi;
(iv) Kuratibu mazungumzo, makubaliano ya pande mbili na zaid ya pande mbili;
(v) Kutunza kumbukumbu za masuala yote ya kisheria;
(vi) Kushughulikia mjumuiko wa makosa; na
(vii) Kutafsiri sheria, na mikataba ya kimataifa na ya ndani inayohusika na shughuli za uvuvi.