Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu

(DSFA)

MAFUNZO YA UVUVI YAHITIMISHWA KWA KISHINDO KUELEKEA TAMASHA LA KIZIMKAZI - ZANZIBAR

Imewekwa: 18 August, 2024
MAFUNZO YA UVUVI YAHITIMISHWA KWA KISHINDO KUELEKEA TAMASHA LA KIZIMKAZI - ZANZIBAR

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Silas Shemdoe akiwahutubia wavuvi 96 wa Kizimkazi Kusini Unguja waliopatiwa mafunzo ya Uvuvi kuelekea Maadhimisho ya Tisa ya Tamasha la Kizimkazi 2024 yatakayofanyika kuanzia tarehe 18 hadi 25.

Prof Shemdoe alikuwa Mgeni Rasmi kwa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 16 Agosti 2024 akimwakilisha Mhe. Abdalla Hamis Ulega (Mb.), Waziri wa Mifugo na Uvuvi. Mafunzo hayo yametolewa na wakufunzi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA), Wakala wa Mafunzo ya Uvuvi Tanzania (FETA), na Wizara ya Bluefish na Uvuvi (WUBU), kwa ufadhili wa DSFA.

Katika hotuba yake Prof.Shemdoe aliwahimiza wavuvi hao kutumia vyema elimu waliyoipata katika kuongeza ufanisi wa shughuli zao za uvuvi,kusimamia na kuhifadhi rasilimali za uvuvi na mazingira yake kwa kutumia zana halali na zinazokubalika kisheria.

Aidha Prof Shemdoe amempongeza Mkurugenzi wa DSFA Dkt Emmanuel Sweke pamoja na wafanyakazi wote kwa kuandaa na kugharamia mafunzo hayo yanayotekeleza azma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk Samia Suluhu Hassan.

Wakisema kuwa baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo wavuvi hao waliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wadau wote waliofanikisha mafunzo hayo na kukiri kuwa yatawasaidia katika shughuli zao za uvuvi.

Mrejesho, Malalamiko au Wazo