Waziri wa Mifugo na Uvuvi afanya ziara Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi afanya ziara Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu
Imewekwa: 30 January, 2025

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amefanya ziara katika Mamlaka ya Kusimamia Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA) na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo. Mhe. Dkt. Kijaji amewataka watumishi wa DSFA kuongeza juhudi katika kufanya kazi ili kuengeza pato la nchi. Mhe. Waziri ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi ya Tanzania Bara Prof. Mohamed Shehe, ziara hiyo imefanyika siku ya tarehe 29/01/2025.