Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi afanya ziara DSFA
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi afanya ziara DSFA
Imewekwa: 16 August, 2024
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Mhe. Shaaban Ali Othman amefanya ziara katika Ofisi za Mamlaka ya Kusimamia Uuvi wa Bahari Kuu (DSFA) na kuzungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo. Mhe. Shaban alipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa DSFA Dkt. Emmanuel Andrew Sweke pamoja na wafanyakazi wote. Aidha Mhe. Shaban aliwataka watumishi wa DSFA kuzidisha ushirikiano katika kutekeleza majukumu yao. Nae Mkurugenzi Mkuu wa DSFA Dkt. Sweke aliwasilisha maelezo mafupi juu ya kazi na majukumu ya Mamlaka hiyo. Mhe. Shaaban aliambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Nd. Zahor Al Kharousy.